Ijumaa, 14 Agosti 2015


RED SEA FC
Vijana hawa ni moja ya mazao HATARI  sana kisoka ndani ya Kigamboni yetu ila kutokana ka usimamizi mbovu wa kimichezo wengi wamejikuta wakiachana na soka na kufanya kazi zao binasfi.. Michezo ni ajira inayowapa fursa vijana kujikwamua KIMAENDELEO tusidharau hilo..

Nisiongee mengi acha niwape list ya kikosi;
1.SHUKURU
2.UNKNOWN
3.JACK
4.EDDY
5.CHII
6.KIZA
7.CHAIJABA
8.MABE
9.NYAMBI
10.KIDISHI SWEDI
11.KABUGO

Vijana wanajituma kwa moyo sana tafadhalini tuungane ili kuwapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao wajikwamue kimaisha

UWANJA WA KUMBUKUMBU YA AL-HAJI ABDU JUMBE(Machava)

unapolizungumzia swala la michezo unazungumzia swala lingine kabisa katika dunia hii. Wapo waliopata vilema,wapo waliofariki,wapo waliacha wake zao na waume pia,wapo waliopata umaarufu,wapo waliopata kazi,wapo waliopata pesa kupitia michezo hii hii.. nashukuru kwa wanaojitolea na kusaidia michezo hasa ndani ya kigamboni yetu na shukran hizi ziende kwa FERRY JOGGING SPORTS CLUB kwa kuweza kukodi mashine ya kukatia nyasi na kusawazisha uwanja wa al-haj abdu jumbe(MACHAVA) na kusawazisha karibu robo ya uwanja mzima bila kujali nani ataenda kucheza pale hii ni changamoto kwa chama cha maendeleo ya michezo kigamboni(KIGAMBONI SPORTS DEVELOPMENT ASSOCIATION) maana toka kikao chao cha mwisho cha trh 3-5-15 mada ikiwa matengenezo uwanja wa al-haj abdu jumbe ambacho kiliamua kuusawazisha uwanja kwa greda mpk leo hamna hatua yoyote iliyochukuliwa huku ikiwaacha wapenzi na wadau wa michezo kigamboni kukosa maeneo ya kufanyia mazoezi kama tunavyojua uwanja wa tippa karibuni utakua ni tatizo kutumika hivyo ongezeko la wanamichezo watakaokua wanatumia uwanja wa machava kutumika.. Mimi naona viongozi wa hiki chama wangejiudhuru maana hawawezi kuwatumikia wanakigamboni ipasavyo.. Michezo ni kazi ambayo imewanufaisha wengi hasa walioitilia maanani na naamini kigamboni ina wanamichezo wengi tu ambao wanandoto za kua wachezaji wa kimataifa bali ndoto zao zinazimwa na watu wachache tu wakati umefika tuone mabadiliko..


PICHAN;shughuli ya ukataji majani ikiendelea

                                                       
A.B.C  FC
Hao ndio AFRICAN BANGI CHAKULA walikua story Kigamboni nzima nani asiye wajua anyooshe mkono juu.. Mimi leo ninachofanya ni kuwakumbusha chama tu ili watoto zetu waenzi timu hizi zilizosababishaga KIGAMBONI kujulikana kimichezo miaka hiyo;
1. ISMAIL TITO
2.TABU
3.MKUDE
4.MTI MKAVU
5.KIDISHI SWEDI
6.ISSA CHIBEDI
7.BEKA 
8.MALOSHO

Wanaharakati tujitahidi kwa nguvu zetu zote ili michezo kigamboni isipotee maana hapa tulipo ni pabaya.. Leo KIGAMBONI haina hata timu ipo ligi daraja la tatu ni vitu vya kuangalia sana kwa makini

ilani: Majina ya baadhi ya wachezaji ni ya utani
SAIGON FC
Vijana walikua hatari hawa balaa cjui cku izi soka la KIGAMBONI kwanini linakufa tunakosa kabisa timu ambazo zilikua zinatukosha wana KIGAMBONI hii ilikua moja ya timu ambazo zilikua balaa kwa kipindi icho.. staki niseme mengi leo acha niwakumbushe tu na kuweka historia kwa watoto wetu wakumbuke chama hili;

1.MAZIKU
2.JOSEPH KIBUBUTU
3.MBONDO
4.NAIJE
5.RAJABU
6.AFIZI NGUMI JIWE
7.JUMA KIBEKU
8.INNOCENT
9.OMARY NJANI
10.KIDISHI SWEDI
11.HAMISI KIBEKU

Kigamboni tunaweza kuleta mabadiliko makubwa kama tutaamua kushirikiana katika kuleta mabadiliko ya kimichezo ndani ya KIGAMBONI yetu pendwa na kuenzi timu hizi zilizopotea...