UWANJA WA KUMBUKUMBU YA AL-HAJI ABDU JUMBE(Machava)
unapolizungumzia swala la michezo unazungumzia swala lingine kabisa katika dunia hii. Wapo waliopata vilema,wapo waliofariki,wapo waliacha wake zao na waume pia,wapo waliopata umaarufu,wapo waliopata kazi,wapo waliopata pesa kupitia michezo hii hii.. nashukuru kwa wanaojitolea na kusaidia michezo hasa ndani ya kigamboni yetu na shukran hizi ziende kwa FERRY JOGGING SPORTS CLUB kwa kuweza kukodi mashine ya kukatia nyasi na kusawazisha uwanja wa al-haj abdu jumbe(MACHAVA) na kusawazisha karibu robo ya uwanja mzima bila kujali nani ataenda kucheza pale hii ni changamoto kwa chama cha maendeleo ya michezo kigamboni(KIGAMBONI SPORTS DEVELOPMENT ASSOCIATION) maana toka kikao chao cha mwisho cha trh 3-5-15 mada ikiwa matengenezo uwanja wa al-haj abdu jumbe ambacho kiliamua kuusawazisha uwanja kwa greda mpk leo hamna hatua yoyote iliyochukuliwa huku ikiwaacha wapenzi na wadau wa michezo kigamboni kukosa maeneo ya kufanyia mazoezi kama tunavyojua uwanja wa tippa karibuni utakua ni tatizo kutumika hivyo ongezeko la wanamichezo watakaokua wanatumia uwanja wa machava kutumika.. Mimi naona viongozi wa hiki chama wangejiudhuru maana hawawezi kuwatumikia wanakigamboni ipasavyo.. Michezo ni kazi ambayo imewanufaisha wengi hasa walioitilia maanani na naamini kigamboni ina wanamichezo wengi tu ambao wanandoto za kua wachezaji wa kimataifa bali ndoto zao zinazimwa na watu wachache tu wakati umefika tuone mabadiliko..
PICHAN;shughuli ya ukataji majani ikiendelea
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni